Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania

ISO 9001:2015 Certified

Bodi na Menejiment ya TASAC yatembelea eneo la mradi wa ujenzi wa kituo cha Kikanda cha Uokoaji katika Ziwa Viktoria.A.

Imewekwa: 19 January, 2024
Bodi na Menejiment ya TASAC yatembelea eneo la mradi wa ujenzi wa kituo cha Kikanda cha Uokoaji katika Ziwa Viktoria.A.

Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), wamefanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi (MLVMCT) katika shughuli ya ujenzi kituo cha Utafutaji na Uokoaji (Regonal Maritime Rescue Coordination Centre) wenye thamani Dola za Kimarekani milioni 1. 8 katika ziwa Victoria mkoani Mwanza siku ya Ijumaa tarehe 22 Desemba, 2023.

Ziara hiyo imejionea Mkandarasi M/s CK Associates Limited kwa ushirikiano na mkandarasi mshauri M/s Oubountu Consulting Limited wamesafisha eneo la mradi lenye mita za mraba 13000 na kuzungusha uzio kwa ajili kuweka usalama wa vifaa vya ujenzi.

Bodi imemwelekeza meneja Mradi Nah. Emmanuel Marijani kushirikiana kwa karibu na mkandarasi ili kufanya kazi kwa viwango na kukabidhi kituo hicho katika muda waliokubaliana kukabidhiana mradi huo ambao ni Novemba, 2024.

Aidha,  bodi imeelekeza kuwa Menejimenti ianze kujipanga kupata wataalam watakaotumika kuendesha kituo hicho kitakapo kamilika.

Mradi utakapokamilika utakuwa na ofisi ya kuwahudumia watoa huduma mbalimbali wanaohusika kwenye mnyororo wa uokoaji ambao ni pamoja na Jeshi la Wananchi la Tanzania Kamandi ya wanamaji, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Police na wadau wengine

Mrejesho, Malalamiko au Wazo