BALOZI WA ANGOLA ATEMBELEA BANDA LA TASAC MAONESHO YA SABASABA
Balozi wa Angola nchini Tanzania, Mhe. Domingos De Almeida Da Silva Coelho, leo Julai 4, 2026, ametembelea banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba) yanayoendelea katika Viwanja vya SabaSaba, jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika banda hilo, Mhe. Coelho alipata fursa ya kufahamishwa kuhusu majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na TASAC katika kusimamia usalama, ulinzi na udhibiti wa uchafuzi wa Mazingira ya bahari utokanao na shighuli za Meli.
Aidha, kuhakikisha usafiri wa majini unakuwa salama kwa abiria na mizigo na pia unakuwa kichocheo kwa maendeleo ya Uchumi wa Tanzania.
Pia Balozi Coelho alielekuwa Shirika linasimamia na kudhibiti huduma za Meli na Bandari kwa kuwasimamia watoa huduma hizo kwa kuwasajili na kusimamia Viwango vya huduma wanazotoa.
Vilevile, alielezwa kuhusu mchango wa TASAC katika kuhakikisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwa njia ya maji zinafanyika kwa kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa, sambamba na juhudi za kuendeleza uchumi wa buluu nchini.
Maonesho hayo yenye kauli mbiu “Hii Kubwa Kuliko” yalianza rasmi tarehe 28 Juni na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 13 Julai, 2026.